Blog

MKAKATI WA KUTOKOMEZA UKEKETAJI NCHINI WAZINDULIWA

Na Mwandishi Wetu Dodoma

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amekemea vikali vitendo vya ukeketeji kwa watoto kike na kuwataka wanaojihusisha na ukatili huo kuacha mara moja.

 Ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akihitimisha hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Taifa wa kutokomeza ukeketaji nchini na kuwataka Wadau wote kuendelea kupambana katika kutokomeza ukeketaji na kuongeza kuwa, Serikali inatambua Mchango wao katika kuwakomboa Mabinti waishio katika mila hizo zilizopitwa na wakati.

 “Ukeketaji si jambo zuri na linawakosesha mabinti fursa kwani wanashindwa kujiamini kabisa,vitendo hivyo ni dhambi na havipo kwenye vitabu vya dini na pia ni uonevu wa hali ya juu hivyo Jamii iachane na vitendo hivo”. alisema Naibu Waziri Mwanaidi

 Aidha Mhe. Mwanaidi amewahimiza wadau kutochoka na kuendelea kupambana vikali dhidi ya vitendo vya ukeketaji ili kuwaepusha Watoto wa kike kufanyiwa vitendo hivyo visivyofaa katika jamii.

 Awali akizingumza katika uzinduzi wa Mkakati huo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu amesema Mila na Desturi za kuwaanda watoto wa kike kuelekea utu uzima zinaweza kufanyika kwenye Jamii bila kufanya Ukeketaji.

 “Kuna mambo ambayo ni mazuri ya kuwaanda vijana lakini kitendo kisichofaa ni ukeketaji, tunayo kazi kubwa ya kufanya ambayo ni kubadili fikra za jamii na ikiwezekana kutafuta namna mbadala ya kuendeleza Mila na Desturi zetu,”

 Akiwasilisha Mpango kazi wa kutekeleza Mkakati huo kwa Wadau walioshiriki uzinduzi, Meneja Mradi wa kutoa elimu kuhusu Ukeketaji na afya ya uzazi wa Shirika la AMREF HEALTH AFRICA, Dkt. Jane Semfano amesema vitendo vya Ukeketaji nchini vimepungua huku akionesha takwimu za 1996 ilikuwa ni asilimia 18 na utafiti wa mwaka 2015/16 ulionesha kwamba msichana mmoja kati ya 10 ndiyo amekeketwa.

Mmoja wa Mangariba aliyestaafu kazi hiyo kutoka Mkoa wa Singida Hawa Hussein amesema kitendo hicho ni hatari kubwa kwa sababu ameshuhudia madhara mengi ikiwemo vifo kupitia mikononi mwake hivyo amewaasa Mangariba wote kuacha vitendo hivyo.

 “Ninawasaidia wamama wengi kujifungua zaidi ya 200 pamoja na kuwapa elimu ya kuacha kuwakeketa watoto wadogo, nimeshuhudia hili jambo ni baya, wanatoka damu nyingi sana” amesema Hawa.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akihitimisha hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa kutokomeza ukeketaji nchini iliyofanyika Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu  akizindua Mkakati wa Taifa wa kutokomeza Ukeketaji nchini katika hafla iliyofanyika Jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Taifa wa kutokomeza ukeketaji wakifuatilia hotuba ya mgeni Rasmi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Kimila na Machifu kabla ya kuhitimisha hafla ya uzinduzi wa mkakati wa kutokomeza Ukeketaji nchini iliyofanyika jijini Dodoma.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WAMJW

Article first published onhttps://issamichuzi.blogspot.com/2021/11/mkakati-wa-kutokomeza-ukeketaji-nchini.html

Amref Health Africa

Amref Health Africa teams up with African communities to create lasting health change.

Recent Posts

When Water Arrived, Everything Changed

When Frederik Lokeun looks across the grounds of St. Matthews Nadome Primary School near Kakuma…

22 hours ago

Mind the Gap on Ebola: It’s the People, Not Just the Virus

The influx of people, equipment and supplies needed to respond to the Ebola virus outbreak…

3 days ago

Sustainability Needs Solidarity: Lessons from Ebola

The current Ebola outbreak in East Africa is a stark reminder of how far the…

6 days ago

Strengthening Community Health Actors to Sustain Immunisation Gains in Burkina Faso

We have seen this happen way too many times in health systems; national policies are…

7 days ago

Closing Immunisation Gaps in Kenya: Reaching Zero-Dose Children in Last Mile Communities

Kenya has made tremendous strides in reaching zero-dose children through a system-wide shift driven by…

1 week ago

When Listening to Health Workers Changed Everything in Nigeria

Sometimes the biggest breakthroughs in health programmes do not come from new technologies or larger…

1 week ago