NAIBU WAZIRI WA AFYA DKT. MOLLEL AKABIDHI VYANDARUA KWA WANAWAKE SHINYANGA MJINI

by Amref Health Africa

Katika kuadhimisha siku ya Malaria Duniani, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ameungana na mwenyeji wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe Pascal Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kugawa vyandarua kwa wanawake zaidi ya 400 pamoja na kufikia makundi mbalimbali ya wananchi katika jamii ndani ya Manispaa ya Shinyanga.

Dkt. Mollel ameipongeza Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Amref kuja na mkakati huo wa kuwafikia wananchi moja kwa moja na kuweza kutoa misaada mbalimbali inayogusa maisha ya Watanzania.

Naibu waziri wa afya dkt. Mollel akabithi vyandarua kwa wanawake Shinyanga mjini

Katika Warsha iliyohudhuriwa na wanawake zaidi ya 400, Dkt. Mollel amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imelenga kuboresha huduma za uzazi, mama na mtoto na kuhakikisha jamii inapata elimu ya kutosha na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

“Asante wakina mama mliokuja hapa kupata elimu ili mkatusaidie kuelimisha wengine na kupunguza vifo vya akina mama na watoto” amepongeza Dkt. Mollel

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Doris Mollel Bi. Doris Mollel amesema kuwa lengo la warsha hiyo ni kutoa elimu ya ugonjwa malaria na namna ya kujikinga pamoja na kuhamasisha wanawake kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO-19 ili waweze kujikinga janga hili kubwa la korona, tunaliona linaisha ila bado ugonjwa upo.

“Zoezi limefanyika katika mikoa mitatu kwa kushirikiana na Amref kwa mikoa ya Simiyu, Kagera na Shinyanga na tunaishukuru Serikali kwa kutuwekea mazingira wezeshi sisi taasisi binafsi kuweza kufanya kazi na kutoa mchango wetu ndani ya jamii” amesema Doris Mollel.

Article first published on https://issamichuzi.blogspot.com/2022/04/naibu-waziri-wa-afya-dkt-mollel.html

You may also like

Leave a Comment

* By using this form you agree with the storage and handling of your data by this website.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More